Arteta akataa kumuuza Nketiah

15Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Arteta akataa kumuuza Nketiah

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amekanusha uwezekano wa Eddie Nketiah kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo katika miezi sita ya mwisho ya mkataba wake hapo kwenye Uwanja wa Emirates na anaaminika kuwa kwenye mazungumzo ya kuhamia Crystal Palace.

Mara baada ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la EFL dhidi ya Liverpool juzi ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana, Arteta alisisitiza nyota huyo raia wa England hataelekea kwingine wakati wa majira haya ya baridi.

“Hali ni kwamba Eddie ni mchezaji wetu na atabakia hapa kwetu. Ni mchezaji wetu na yuko chini ya mkataba, kwa hivyo atakuwa nasi,” alisema Arteta akiwaambia waandishi wa habari

Nketiah amefunga mara tano kwenye mechi tatu za Kombe la EFL msimu wa 2021-22, lakini amecheza dakika 38 pekee kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Kinda huyu wa Uingereza anajivunia jumla ya mabao 18 na asisti moja katika mechi 72 akiwa na Arsenal akitokea katika akademi yao.

Habari Kubwa