Augua ghafla ngiri akishangilia bao

18Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
LONDON, England
Nipashe
Augua ghafla ngiri akishangilia bao

WAKATI mwingine ushabiki wa mchezo wa soka ni kama utumwa unaoweza kusababisha madhara makubwa, kikiwamo kifo.

ARSENAL

WAKATI mwingine ushabiki wa mchezo wa soka ni kama utumwa unaoweza kusababisha madhara makubwa, kikiwamo kifo.

Shabiki mmoja wa Arsenal amelazwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji baada ya kuugua ghafla wakati akishangilia bao la ushindi la timu yake.

Shabiki huyo aliyetajwa kwa jina la Scott Woods, alishikwa na ugonjwa wa hernia (ngiri) wakati akishangilia bao lililofungwa na mshambuliaji Danny Welbeck kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City.

Akitokea benchi, Welbeck alifunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Kilichomponza shabiki huyo ni kushangilia bao hilo kupita kiasi na kesho yake alijikuta akiwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa hernia.

Nilikuwa naruka kwa furaha jirani na alipokaa baba yangu na kumkumbatia.Nilijisikia vibaya Jumatatu na nikalazimika kwenda hospitali katikati ya usiku; alisema shabiki huyo.

Baada ya tukio hili nitakuwa makini na nitakuwa mpole, alisema Scott baada ya kuulizwa atawezaje kwenda sambamba na afya yake iwapo Arsenal watatwaa ubingwa wa England.