Aussems aanza mikakati kuimaliza As Vita

14Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Aussems aanza mikakati kuimaliza As Vita

BAADA ya juzi timu yake nkuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua yamakundi ya ligi yamabingwa Afrika, kocha wa Simba, Patrick Aussems, amesema kwa sasa nguvu zao wanaelekeza kwenye mchezo dhidi ya AS Vita.

Smba sasa inajiandaa kuumana na timu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao juzi usiku walipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye kundi lao la D dhidi ya Al Ahly baada ya kufungwa mabao 2-0.

Akizungumza jana, Aussems, alisema wachezaji wake wamefanya kazi kubwa kwenye mchezo wa juzi na walifuata maelekezo yake.
Alisema atafanyia kazi mapungufun madogo aliyoyaona kwa ajili yakujiandaa dhidi ya As Vita.

“Mchezo wa kwanza umepita, kwa sasa tutaanza maandalizi ya mchezo wetu unaofuata, lengo ni kuona tunafanya vizuri kwenye kundi, yapo mambo madogo ninayotakiwa kuyafanyia kazi kabla ya mchezo wa pili” alisema Aussems.

Aidha, alisema nagependa kuona nyota wake wawili John Bocco na Erasto Nyoni ambao ni majeruhi wanapona haraka na kurejea kikosini.

“Bocco alishindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu ya mguu, bado sijajua undani wa maumivu yake, lakini ningependa kuona anarejea kikosini mapema,” alisema Aussems.

Bocco juzi alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Medy Kagere ambaye aliifungia Simba mabao mawili kwenye ushindi huo.

Matokeo ya jumla yanaifanya Simba kuongoza kundi lao wakiwa na pointi tatu sawa na Al Ahly lakini wekundu hao wa Msimbazi wana mabao matatu moja zaidi ya Al Ahly.

Habari Kubwa