Aussems: Tupo tayari kuivaa Azam

22Oct 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Aussems: Tupo tayari kuivaa Azam

TUMEIMARIKA! Hayo ni maneno ya Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Patrick Aussems, kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam FC, unaotarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Aussems alisema kuwa kikosi chake kimejiandaa vema kuwakabili Azam FC na mechi za kirafiki walizocheza, zimesaidia kuwaweka imara kuwavaa wapinzani hao.

Kocha huyo alisema kwamba wamejiandaa kukabiliana na ushindani katika mchezo huo kutokana na ubora walionao wachezaji wa Azam FC.

"Tuko tayari kwa mchezo huo, ni mchezo muhimu na utakaokuwa na ushindani, Azam ni timu nzuri, tunalijua hilo," alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Kipa Beno Kakolanya, alisema kuwa licha ya kuwafunga Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii, wamejipanga kupambana ili kuendeleza rekodi yao ya ushindi msimu huu.

"Ni kweli mechi iliyopita tuliwafunga, lakini Azam si wabaya, walitupa ushindani katika muda wote wa mchezo," Kakolanya aliongeza.

Habari Kubwa