Azam FC wajifua kwenye mvua Sauzi

11Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Azam FC wajifua kwenye mvua Sauzi

WACHEZAJI wa Azam FC juzi jioni walilazimika kufanya mazoezi, huku mvua ikinyesha kwa ajili ya kujiandaa kuwakabili wenyeji wao Bidvest Wits katika mechi ya raundi ya kwanza ya mashindano ya Kombe la Shirikisho utakaofanyika kesho Jumamosi jijini Johannesburg.

Wachezaji wa Azam FC wakiwa uwanja wa ndege tayari kwa safari.

Taarifa zilizopatikana katika mtandao wa klabu hiyo jana, zimeeleza kuwa baada ya kukaa kwa zaidi ya saa moja kusubiri mvua imalizike, kocha Stewart Hall aliwataka wachezaji wake kufanya mazoezi katika hali hiyohiyo kwenye Uwanja wa Chuo cha Wits.

"Kikosi cha Azam FC kilifanya mazoezi yake ya kwanza kuanzia saa 11.50 jioni ya leo (juzi) kwa takribani saa moja na robo kwenye Uwanja wa timu ya Chuo cha Wits jijini Johannesburg. Wachezaji walifanya mazoezi huku mvua ikinyesha," alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Bara msimu 2013/ 14 watashuka kuikabili Bidvest Wits iliyo katika nafasi ya pili Ligi Kuu Afrika Kusini.

Habari Kubwa