Azam FC yatamba kuendeleza ubabe

19Jul 2019
Shufaa Lyimo
Dar es Salaam
Nipashe
Azam FC yatamba kuendeleza ubabe

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche, amesema kuwa watashuka uwanjani kuwavaa AS Maniema ya Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Kagame ili kulinda heshima ya Tanzania.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche, alisema kuwa wanajua mchezo huo utakuwa mgumu, lakini tayari wameshawasoma wapinzani wao na wamejipanga kuwakabili.

"Mchezo wa nusu fainali huwa ni mgumu, ni mchezo unaohitaji tahadhari, unahitaji kujilinda zaidi kwa sababu hauna marudio, tumejiandaa vizuri ili kuipa heshima timu yetu na nchi yetu, vijana wote tuliokuwa nao hapa wako vizuri," alisema Cheche ambaye ni Msaidizi wa Mrundi Etienne Ndayiragije.

Mechi nyingine ya hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itakayochezwa leo itakuwa ni kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya Green Eagles kutoka Malawi.