Azam hakuna kulala, fasta waifuata Mwadui

23Apr 2016
Somoe Ng'itu
Dar es Salaam
Nipashe
Azam hakuna kulala, fasta waifuata Mwadui

AZAM FC wameasili Dar es Salaam jana wakitoka Tunisia walikokwenda kushiriki michuano Kombe la Shirikisho dhidi ya Esparance na kuunganisha moja kwa moja Mwanza tayari kwa mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage Stadium in Shinyanga.

timu ya Azam.

Azam iliondolewa kwenye mashindano hayo baad aya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji wao katika mechi ya marudiano, hivyo kufungwa jumla ya mabo 4-2 baada ya wawakilishi hao Tanzania kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini zaidi ya wiki moja iliyopita.

Msemaji wa Azam FC, Jaffer Iddi alisema jana kuwa wameamua kuunganisha ndege kwenda moja kwa moja Mwanza kwa sababu hawana muda wa kutosha.

Alisema wachezaji wawili walioshindwa kusafiri na timu hiyo kwenda Tunisia kwa sababu ya kuwa mejeruhi, wamepata nafuu na wameungana na wenzao kwa safari ya Mwanza. Wachezaji hao ni mlinzi, Pascal Wawa na mshambuliaji Kipre Tchetche.

“Wachezaji wamewasili leo na mchana huu (jana) wanaunganisha ndege kwenda Mwanza. Hakuna mchezaji atakayekwenda nyumbani kwa ajili ya mapumziko kwa sababu tunataka kushinda mechi dhidi ya Mwadui," alisema Idd.

Habari Kubwa