Azam: Tumekuja kuwapiga Toto

03Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Mwanza
Nipashe
Azam: Tumekuja kuwapiga Toto

WAKATI leo wanamenyana na wenyeji, Toto African Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Azam FC wamesema waamefuata pointi tatu mjini humo katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kocha Azam, Stewart Hall.

Akizungumza na Lete Raha jana mjini Mwanza, Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema kwamba wamekuja mjini hapa kwa lengo moja tu la kuchukua pointi tatu katika mchezo huo.

“Ligi imefikia sehemu muhimu sana, kukusanya pointi ni jambo la msingi sana, tukishinda mechi zetu zote zilizobakia tuna uhakika na ubingwa wa ligi, hivyo tumelenga pointi tatu dhidi ya Toto,” alisema Hall.

Azam FC ambayo itamkosa beki wake majeruhi, Gardiel Michael anayeendelea na matibabu ya goti imefikia katika Hoteli ya Mipa mjini hapa na jana wamefanya mazoezi Uwanja wa CCM Kirumba.

Azam FC kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 50 sawa na Yanga iliyo juu yake, lakini timu zote hizo zimezidiwa mechi tatu na Simba inayoongoza ligi kwa pointi 57.

Habari Kubwa