Azam yaweka kambi Pretoria

17Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Azam yaweka kambi Pretoria

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC wameweka kambi fupi kwenye jiji la Pretoria nchini Afrika kusini kabla ya kuelekea Swaziland kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows.

Azam wanatarajia kurudiana na wenyeji wao Mbabane Swallows Jumapili saa 9:30 mchana kwa saa za Swaziland ambayo ni sawa na Saa 10:30 kwa saa za Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, aliiambia Nipashe kutoka Pretoria kuwa wameamua kusimama jijini humo kwa ajili ya kujaribu kuzoea hali ya hewa ambayo inafanana na Swaziland.

"Tunaweza tukaondoka hapa Ijumaa au Jumamosi kuelekea Swaziland kwa ajili ya mchezo wetu na Mbabane Swallows," alisema Kawembwa.

Azam inahitaji ushindi au sare yoyote ili kuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

Habari Kubwa