Barthez, Dida yoyote kuwavaa Waarabu

05Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
Barthez, Dida yoyote kuwavaa Waarabu

KOCHA wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali amesema kuwa yeyote atakayekuwa fiti zaidi kati ya Ally Mustapha 'Barthez' au Deogratius Munishi 'Dida' ndiye atakayedaka mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly ya Misri Jumamosi.

Ally Mustapha 'Barthez'.

Kocha huyo alisema kuwa kwenye kikosi chake hakuna kipa namba moja wala mbili, kwani wote ni makipa bora na waliokamilika.

"Naweza kuwashangaza watu Jumamosi wakaona mabadiliko golini, hii ni kwa sababu ninapowafundisha makipa huwa nataka wote wawe kwenye kiwango kinachofanana," alisema.

Yanga ni moja kati ya timu chache ambazo hubadilisha makipa mara kwa mara kwenye mechi za ligi.

Kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014, Dida alidaka mechi zote mbili ya Dar es Salaam, Yanga ikishidna 1-0 na ile ya marudiano mjini Cairo ilipofungwa bao 1-0 na kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3, huku kipa huyo aking'aa kwa kuokoa penalti mbili.

Wakati kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Ndanda, Yanga ilimuweka Dida golini, lakini kwenye mechi ya mwisho kabla ya kuwavaa Waarabu, Barthez alikaa golini.

Habari Kubwa