Bashungwa atarajiwa kufungua mashindano ya Umisavuta 2021

05Dec 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Bashungwa atarajiwa kufungua mashindano ya Umisavuta 2021

WAZIRI wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Innocent Bashungwa, leo Desemba 5, anatarajia kufunga rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu (Umisavuta) 2021.

WAZIRI wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Innocent Bashungwa.

Mashindano ya Umisavuta yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yalianza Novemba 29 mkoani hapa kwa kushirikisha washiriki zaidi ya 800 wakiwemo wanamichezo, waratibu na wadau wengine.

Mwenyekiti wa Walimu wa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara, Doroth Mhaiki, amesema kuwa Bashungwa atakabidhi medali kwa bingwa wa soka wa mashindano hayo kwenye mchezo utakaochezwa leo katika uwanja wa Nangwana Sijaona mkoani hapa kati ya Kanda ya Mashariki na Kanda ya Kaskazini.

Mbali na kukabidhi medali kwa bingwa soka wa michuano hiyo, pia Bashungwa atashuhudia burudani kutoka kwa washindi wa jumla wa kwaya, ngoma za asili na maigizo ambayo ni sehemu ya michezo iliyoshindanishwa tokea kuanza kwa mashindano hayo ya Umisavuta.

Habari Kubwa