Betway yazindua kituo cha michezo Tanzania

15Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Betway yazindua kituo cha michezo Tanzania

KAMPUNI ya Kimataifa ya Michezo ya Kubashiri (Betway), imechukua hatua kubwa katika kuongeza thamani kwenye sekta ya michezo nchini Tanzania baada ya kuzindua kituo cha kisasa cha kushuhudia michezo na kubashiri kistaarabu ‘Betway Sports Experience Center’.

Meneja wa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya kubashiri yalioendeshwa na Betway wakati wa uzinduzi wa kituo cha kushuhudia michezo - 'Dimba la Betway".

Kituo hicho cha kipekee na cha aina yake ambacho kitakuwa sehemu maalum ya kuwakutanisha wapenzi wa michezo kushuhudia michezo mbalimbali na kufanya ubashiri katika mazingira ya kuvutia, kimepewa jina la Dimba la Betway ambapo kitakuwa pia kikitoa elimu kuhusu michezo na namna ya kubashiri kistaarabu.

 

Katika kituo hicho ambacho kipo ndani ya ofisi za Betway zilizopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, kimewekwa vifaa vya kisasa ikiwamo simu janja na kompyuta maalumu kwa ajili ya wateja kujisajili na kufanya ubashiri wa michezo inayoendelea mubashara huku kikiwa kimefungwa 'skrini' maalumu za runinga zinazoonyesha michezo mubashara inayochezwa kwa wakati huo na kutoa nafasi kwa wateja kufuatilia matokeo ya mechi hizo.

 

Aidha, kituo hicho kinatoa nafasi kwa wateja kucheza michezo ya kasino na mingine ya ubashiri huku wakipata fursa ya kuuliza maswali, kusajili akaunti mpya, na kufanya ubashiri kwa kutumia simu na kompyuta zilizopo ndani ya kituo.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe, alisema uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuongeza thamani katika sekta ya michezo nchini.

 

"Sisi (Betway) tuna furaha kubwa kuzindua kituo hiki cha kipekee na muhimu kwa mashabiki wa michezo Tanzania kuweza kukutana na kufurahia kwa pamoja na kwenye mazingira ya kuvutia.

 

Hii ni sehemu ya ahadi yetu - kuongeza thamani katika michezo ya kubashiri na sekta ya michezo kwa ujumla kwa sababu kituo hiki kitakuwa kama kitovu cha michezo ambapo mashabiki wataweza kukutana, kutazama michezo, na kufanya ubashiri wao kwa njia bora ambayo haijawahi kutokea hapo awali," alisema.

 

Akizungumza na wadau wa michezo pamoja na wanahabari waliohudhuria tukio la uzinduzi, Jimmy alisema Betway inafanya kazi kutimiza ahadi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini Tanzania kama ilivyoahidi wakati ikiingia nchini na kuwahakikishia wote kuwa Kampuni hiyo itaweza kuwaongoza wateja wake katika kuiishi na kuitimiza kauli mbiu ya "Bashiri Kistaarabu" kwa kuwaonyesha wateja wake kwa vitendo.

 

Habari Kubwa