Cannavaro aionya Mbeya City FC

09May 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Cannavaro aionya Mbeya City FC

NAHODHA wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameitahadharisha Mbeya City kujiandaa na kipigo katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara watakayokutana kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

CANNAVARO

Akizungumza na gazeti hili jana, Cannavaro, alisema mechi hiyo ushindi dhidi ya Sagrada Esperanca walioupata ni kipimo dalili njema kwao wataibuka na ushindi na kutetea ubingwa waliokuwa wanaushikilia.

“Hizi ni salamu kwa Mbeya City, wajipange vizuri kwa sababu tunaenda kuchukua pointi tatu ambazo zitatufanya Yanga kutembea kifua mbele, tumejipanga kutangaza ubingwa kwa heshima," alisema Cannavaro.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuwasili Mbeya asubuhi ya leo kwa usafiri wa ndege na baada ya hapo kitasafiri kuelekeza Mtwara kuikabili Ndanda FC katika mechi nyingine ya ligi hiyo.

Habari Kubwa