Carroll tatu, Arsenal tatu

10Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Carroll tatu, Arsenal tatu

MSHAMBULIAJI wa West Ham United, Andy Carroll, jana alifunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Upton Park jana.

arsenal

Matokeo hayo ni mabaya kwa Arsenal katika safari ya kusaka ubingwa England msimu huu, kwani sasa wako nyuma kwa pointi 10 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Leicester City, huku mechi sita zikisalia kabla ya ligi kumalizika.

Mesut Ozil na Alexis Sanchez walifunga mabao kutokana na 'asisti za Alex Iwobi na kufanya matokeo kuwa 2-0, lakini Carroll alifunga mara mbili katika muda wa sekunde 160 na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mapumziko.

Carroll alimaliza hat trick yake katika dakika ya 52, kabla ya Laurent Koscielny kwa Arsena katika dakika ya 70.
Wenyeji wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi kwenye uwanja wa nyumbani kufikia 14, lakini wakibaki nafasi ya sita kwenye msimamo.

Habari Kubwa