Chamba : Sportpesa ndiyo inaning'arisha

25Nov 2018
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Chamba : Sportpesa ndiyo inaning'arisha

TIMU ya uhindi imefika mpaka wilaya ya Ileje, Songwe ambapo wamekutana na mshindi wa droo ya 33, Michael chamba ambaye alibashiri na moja kwa moja kuingia kwenye droo ya Shinda zaidi na SportPesa.

Mshindi wa droo ya 33 ya Promosheni ya Shinda Zaidi na Sportpesa, Michael Chamba (kushoto) kutoka Ileje, Songwe akionyesha funguo ya bajaji baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo aliyoshinda. PICHA : SPORTPESA

Akizungumza na timu ya Sportpesa mara baada ya kukabidhiwa bajaji yake, Chamba alisema aliifahamu SportPesa kupitia mjomba wake ambaye alimuelekeza na yeye kuanza kucheza.

"SportPesa niliifahamu kupitia mjomba wangu baada ya kumuona yeye amecheza na kufanikiwa kushinda zaidi ya shilingi milioni mbili iliyomuwezesha kununua bodaboda yake mpya ndipo na mimi nilipata ushawishi na kuanza kucheza mwisho wa siku hatimaye nimebahatika kushinda bajaji, nilichojifunza SportPesa ni kwamba kampuni hii haichagui kila mtu ana nafasi ya kushinda" alisema Chamba.

Akielezea mikakati yake mara baada ya kukabidhiwa chombo chake cha ushindi alisema ataboresha biashara yake ya kuuza chakula na kujenga mgahawa mkubwa wa kisasa na kuachana na kibanda anachotumia hivi sasa, kingine ni kumsomesha mtoto wake ambaye amefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Aidha mipango yake mingine ni kuhakikisha anawasaidia ndugu zake ambao hawajiwezi kiuchumi, huku akihaidi kuweka usimamizi mzuri kwa kila kipato kitakachoingia kutokana na bajaji.

Ndoto kubwa ya Chamba iliyobakia hivi sasa ni kushinda jackpot ambapo ameiahidi timu ya ushindi ijiandae kurudi kwa mara nyingine ileje ambapo safari ijayo itakuwa kumpelekea mamilioni ya Jackpot.

Bado SportPesa wanakuhakikishia kwamba kucheza ndio kushinda na hapa unaweza kushinda bajaji au mamilioni ya Jackpot au unaweza kushinda Vyote kwa pamoja hii ni kupitia simu yako ya mkononi unabofya *150*87# unajisajili kisha unaweka pesa na kuanza kucheza.

Habari Kubwa