Cheka aanza kujifua

12Mar 2016
Dar
Nipashe
Cheka aanza kujifua

BONDIA Francis Cheka anatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo kujiandaa dhidi ya bondia kutoka Colombia.

Waziri wa Habari, Nape Nnauye akijaribisha kuvaa mkanda wa ubingwa wa Bondia Francis Cheka.

Cheka anayeshikilia mkanda wa ubingwa wa mabara, anatarajia kuzichapa na bondia huyo Juni mwaka huu katika pambano la raundi 12 uzito wa Kati.

Akizungumza na gazeti hili jana, Cheka alisema anajiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo.
“Nataka kufanya mazoezi ya nguvu tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza,” alisema Cheka.

"Safari hii, ninaanza mazoezi mapema, ikiwemo kupima uzito mara kwa mara ili kuepuka kuzidisha uzito zaidi ya unaotakiwa."

Alisema kutokana na shida aliyoipata katika pambano la awali, safari hii hatafanya tena makosa.

Habari Kubwa