Courtois aishutumu FIFA, UEFA

14Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Courtois aishutumu FIFA, UEFA

GOLIKIPA wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois amelishutumu Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA), na ile la Ulaya (UEFA), kwa kutojali tena wachezaji, baada ya kuongezeka kwa mashindano mengi na kuhoji umuhimu wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Ligi ya Uefa.

Ubelgiji ilicheza na Italia katika kutafuta mshindi wa tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa ya Uefa, ambapo ilifungwa, kabla ya mchezo wa fainali ambao ulizikutanisha Ufaransa na Hispania.

Na sasa Courtois ameishutumu FIFA na UEFA kwa kujali fedha pekee.

“Ni mchezo wa fedha tunapaswa tuwe wakweli kuhusu hili,” alisema Courtois akiwaambia waandishi wa habari.

“Tumecheza huu mchezo ni kwa sababu ya UEFA, fedha ya ziada na mchezo wa ziada kwenye TV.

“Tutapata majeraha, hakuna anayejali wachezaji, baada ya msimu mrefu unatakiwa tena kucheza Ligi ya Uefa na utakuwa na wiki mbili za mapumziko hiyo haitoshi kwa wachezaji.

“Wanaweza kuchukizwa na Super League, lakini hawajali kuhusu wachezaji wanajali mifuko yao tu. Sisi siyo maroboti.”

Habari Kubwa