Coutinho: Nimekuja Villa kurudisha makali yangu

15Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Coutinho: Nimekuja Villa kurudisha makali yangu

KIUNGO wa Barcelona, Phillipe Coutinho aliyehamia Aston Villa kwa mkopo wa miezi sita amesema kocha wa timu hiyo, Steven Gerrard ndiye aliyemshawishi kuhamia huko ili aweze kurejesha makali yake.

Coutinho ambaye ameshindwa kupata nafasi katika kikosi cha Barcelona, amekamilisha uhamisho wake wa kuichezea Aston Villa mpaka mwisho wa msimu siku ya Jumanne huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa kiasi cha pauni milioni 33 kipindi cha majira ya joto.

Akielezea uamuzi wake wa kuhamia Aston Villa, Coutinho aliiambia BBC Sport: “Steven Gerrard aliniambia kuhusu klabu, shauku na mipango ya yake kwenye klabu.

“Nilipozungumza naye baada ya kikao ilikuwa wazi anataka nije hapa, nadhani imekuwa haraka na nafurahi kuwa hapa.

Coutinho alikuwa anahitaji kurudi katika Ligi Kuu England na kucheza mara kwa mara na aliona Aston Villa kama klabu sahihi ambayo inaweza kutengeneza kitu kizuri hapo baadaye.

Habari Kubwa