Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF), jana ikisainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wake, Cliford Ndimbo, imetahadharisha kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha hilo kufungwa.
"Dirisha la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Championship, 'First League', na Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2022/23 litafunguliwa Julai Mosi na kufungwa Agosti 31, mwaka huu.
"Katika kipindi hicho klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa kimataifa. Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana na changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.
"Aidha dirisha dogo, lenyewe litafunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kufungwa Januari 15, 2023," ilihitimisha taarifa hiyo.