Dk Ndumbaro aahidi kuhamasisha Mawaziri kujifunza gofu

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Dk Ndumbaro aahidi kuhamasisha Mawaziri kujifunza gofu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro, aahidi kutumia ushawishi wake kuwahamasisha Mawaziri wenzake pamoja wa watu kawaida kujifunza mchezo wa gofu kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa Mabalozi na Wataalamu wa nchi mbalimbali ambao ni wachezaji na wananchama wam chama cha gofu nchinin baada ya kumalizika kwa mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania yaliyofanyika mwezi April mwaka huu mkoani Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu imefanyika nyumbani kwa Balozi Frederic Clavier na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.

Kufuatia ombi la Balozi huyo amesema mbali ya kuwahasisha Mawaziri pia atawahamasisha Wabunge kujifunza mchezo huo ili kuwa timu bora ya Bunge ya mchezo wa gofu hali itakayopelekea Wabunge hao kuendeleza mchezo huo katika majimbo waliyotoka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Dk. Ndumbaro amewapongeza Washiriki hao na kuwaaahidi kuendeleza mchezo huo kwa kuunganisha na utalii wa michezo ili kuhamasisha Mabalozi hao kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

Habari Kubwa