DONDOO KOMBE  LA DUNIA 2018

06Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
DONDOO KOMBE  LA DUNIA 2018

KUNDI A
Wenyeji, Urusi watakabiliana na kazi kubwa kuwazuia nyota wa Misri, Mohamed Salah na wa Uruguay, Luis Suarez. Urusi itafungua michuano hiyo kwa kucheza dhidi ya Saudi Arabia Juni 14.

KUNDI BIran na Morocco ni timu mbili ambazo zinaonekana zinaweza kulifanya Kundi B kuwa na mbinu za kijanja, lakini kutakuwa na ‘derby’ (mechi ya mahasimu) Hispania na Ureno, ambao watakuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutinga hatua ya mtoano.

KUNDI CKwa kuwa mkweli, unaweza kuikingia kifua Ufaransa katika kundi hili linalozijumuisha Australia, Peru na Denmark, kuweza kufanya vizuri na kusonga mbele bila tatizo.

KUNDI DLikiwa na Argentina, Iceland, Croatia na Nigeria, hili litakuwa ni moja ya kundi gumu katika raundi ya kwanza. Kamwe huwezi kuegemea sana kwa Argentina katika michuano mikubwa, lakini bado wanaweza kuwa kinara wa kundi hili ingawa Lionel Messi atahitaji msaada.

KUNDI EUswisi, Costa Rica na Serbia, zitaanza kwa kasi katika kundi hili, lakini usisahau kuwa Brazil haitataka kufanya makosa.

KUNDI FBingwa mtetezi Ujerumani haitaogopa yeyote. Kufuzu kwao imekuwa ni jadi baada ya kutinga michuano hiyo ikishinda mechi 10, na kwa kuutwaa ubingwa wa Kombe la Mabara haitakuwa na chakuhofu dhidi ya Mexico, Sweden na Jamhuri ya Korea.

KUNDI GKama lilivyo Kundi B kwa kuundwa na Hispania na Ureno, kundi hili lina England ambayo itatakiwa kukabiliana na Ubelgiji ya kina Eden Hazard, Kevin De Bruyne na Romelu Lukaku. Lakini mchambuzi, Stewart Robson anaipa nafasi England.

KUNDI HHili ni kundi la kushuhudia vipaji kutoka Poland, Senegal, Colombia na Japan na zote zikipewa karibu nafasi sawa ya kutinga hatua ya mtoano.

 

Habari Kubwa