Droo Kombe la Shirikisho 'live' kesho

02Mar 2016
Somoe Ng'itu
Dar
Nipashe
Droo Kombe la Shirikisho 'live' kesho

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kesho litachezesha droo ya mechi za hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho, Nipashe imebaini.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Bingwa wa mashindano hayo, ataiwakilisha Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Habari za ndani zinadai kuwa, droo hiyo itaonyeshwa live na kituo cha televisheni kinachodhamini mashindano hayo.
"Droo itachezeshwa Alhamisi, itakuwa 'live' katika kipindi cha Alasiri," kilisema chanzo chetu.

Timu nane zimefuzu hatua hiyo, ambazo ni Simba, Yanga, Azam FC, Coastal Union, Ndanda FC, Mwadui FC , Prisons zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara na Geita Goldmine FC ya Ligi Daraja la Kwanza.

Habari Kubwa