Dua atoa somo kumkaba Ngoma

22Apr 2016
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Dua atoa somo kumkaba Ngoma
  • ...Mshambuliaji huyo kutoka Zimbabwe ana tabia ya kuegemea mabeki na kutumia nguvu...

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na timu ya Taifa (Taifa Stars), Dua Said amesema kuwa mabeki wengi nchini wana udhaifu kumkaba mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma.

mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na Beki wa timu hiyo Kamusoko wakishangilia.:picha ya maktaba.

Akizungumza na gazeti hili jana Dar es Salaam Dua alisema mabeki wengi wa kisasa wamekuwa wakimkaba mshambuliaji huyo kwa kushindana naye kitu ambacho anadai hawataweza kuhimili nguvu zake.

Mshambuliaji huyo aliyeng'ara wakati anacheza aliongeza kuwa anawapa ushauri wa bure mabeki kuwa wanapokabana na Ngoma wasishindane kwa nguvu na wala wasikubali awaegemee mwilini.

"Ngoma ana tabia ya kumuegemea beki na kutumia nguvu, lakini mabeki wengi wamekuwa wakikubali kuegemewa jambo ambalo huwagharimu," alisema na kuongeza.

"Zamani kulikuwa na washambuliaji wengi wenye nguvu na wenye uwezo mkubwa kuliko hata Ngoma, lakini walikutana na mabeki wanaotumia akili, wao kazi yako mguu unafuata mpira tu basi," Dua alisema.

Kumekuwa na mlalamiko kutoka kwa makocha wa timu mbalimbali kuwa Yanga imekuwa ikibebwa kwa mabeki wanaocheza dhidi ya mabingwa hao watetezi na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Habari Kubwa