EATV yadhamini usiku wa Valentine

12Feb 2016
Faustine Feliciane
Nipashe
EATV yadhamini usiku wa Valentine

KITUO cha Televisheni cha na Radio cha East Afrika (EATV na Radio) cha Dar es Salaam, kimedhamini onyesho maalum la Sikukuu Valentine kwenye Ukumbi wa King Solomon Jumamosi wiki hii.

Mratibu wa onyesho hilo kutoka Kampuni ya King Solomon, Hellen Kazimoto alisema kuwa EATV na Redio wamedhamini onyesho hilo ilikutoa nafasi kwa wapendanao kuwa pamoja siku hiyo.

"Tunawashukuru EATV na Redio pamoja na wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini onyesho hili la aina yake," alisema Hellen.

Alisema kuwa mwanamuziki nyota wa muzikiwa kizazi kipya, Ben Pol na mkongwe wa muziki wa Taarabu, Patricia Hilary watatoa burudani.

Kwa upande wake, mwakilishi wa EATV na Radio, Yohana Fundi aliwataka wapenzi wa vituo hivyo kujitokeza kwa wingi kwenye onyesho hilo.

Habari Kubwa