Esperance kutua nchini Ijumaa

04Apr 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Esperance kutua nchini Ijumaa

WAPINZANI wa timu ya Azam FC katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, Esperance kutoka Tunisia wanatarajia kuwasili nchini Ijumaa tayari kwa mchezo wao unaotarajiwa kufanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Azam FC, Jaffer Idd.

Msemaji wa Azam FC, Jaffer Idd alisema jana kuwa msafara wa timu hiyo wenye watu 35 utatua saa 4:30 na siku inayofuata itafanya mazoezi yake kwenye uwanja huo utakaotumika Jumapili.

Iddi alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na kuongeza kuwa waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka Afrika Kusini nao watatua nchini Ijumaa.

"Kila kitu kinakwenda vizuri, tunacheza mechi za ligi na mipango ya mchezo wetu dhidi ya Esperance pia imekamilika, kama wenyeji tumehakikisha mambo yote yako sawa," alisema Idd.

Habari Kubwa