FIFA kupambana na rushwa kwenye soka afrika

11Feb 2019
Salome Kitomari
Addis Ababa,Ethiopia
Nipashe
FIFA kupambana na rushwa kwenye soka afrika

Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA), limesema limewekeza nguvu kwenye ulinzi na usalama,kupambana na rushwa na elimu ili kuwezesha mchezo wa mpira kuchangia maendeleo ya Bara la Afrika.

Waziri mkuu kassim majaliwa akizungumza na Rais wa FIFA, Gianini Infantino wakati wa mkutano huo.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika,unaendelea mjini Addis Ababa,Ethiopia, Rais wa FIFA, Gianini Infantino amesema suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana na kwamba kwa FIFA itahakikisha hakuna vifo wala vurugu kwenye mchezo wa mpira.

Amesema pia shirikisho limewekeza nguvu katika kupambana na rushwa ili kuhakikisha mpira huo unakuwa na kwamba watashirikiana na AU kuhakikisha wanafanikiwa.

Aidha, amesema elimu ya mpira pekee haitoshi bali elimu ya kuwasaidia wachezaji kwa kuwa kwenye mpira watajifunza sheria na kanuni lakini kuna elimu nyingine ambayo ni muhimu.

“Kwenye elimu nyingine watajifunza kuwa kuna kushinda na kushindwa,inapotokea wameshindwa kwenye mchezo wowote watatambua kuwa kuna mchezo ujao ambao wanaweza kushinda,” amesema.

Amesema mpira huwa leta pamoja wasomi na watu wa kawaida na ndiyo maana wanafurahi kushirikiana na AU kuhakikisha Afrika inafanya vizuri.

Habari Kubwa