Haonga aamka na Bajaj SportPesa

09Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Haonga aamka na Bajaj SportPesa

PROMOSHENI ya Shinda Zaidi na SportPesa imezidi kuwatoa Watanzania katika dimbwi la umaskini na kujikuta wakiweza kubadili maisha yao kupitia kushinda zawadi kibao ikiwamo bajaj.

Michael Haonga, akionyesha ufunguo wa bajaj baada ya kukabidhiwa na timu ya Ushindi ya SportPesa kufuatia kuibuka mshindi katika droo ya 66. Pembeni ni mkewe na mwanawe pamoja na ndugu jamaa na marafiki walioshuhudia makabidhiano hayo jana. PICHA: SPORTPESA

Katika droo ya 66, Michael Haonga kutoka Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameibuka mshindi wa bajaj mpya kabisa aina ya RE na timu ya ushindi ya SportPesa kumfikishia zawaidi hiyo hadi nyumbani kwake.

Akizungumza na timu ya Ushindi ya SportPesa mara baada ya kukabidhiwa bajaj hiyo, Haonga alisema anashukuru kuona ubashiri wake na SportPesa kwa shilingi 1,000 tu umempa mafaniko ya kushinda bajaj ambayo anaamini itamsaidia kujiimarisha kiuchumi.

"Kupitia bajaj hii sasa nitaweza kulipa kodi ya nyumba kwa wakati, hii ilikuwa ni zaidi ya changamoto kwangu mbali ya hilo nitajitahidi kununua mashine ya kisasa ya kufyatulia tofali maana kazi yangu mimi ni fundi ujenzi," alisema Haonga.

Aidha, Haonga anaamini huu ndio wakati wa yeye kuitwa bosi na kuheshimiwa na jamii inayomzunguka maana atakuwa amempa ajira dereva atakayeendesha bajaj yake.

"Leo nimeamini ule usemi usemao 'lala maskini amka ukiwa tajiri', SportPesa imeniamsha na utajiri, hivi unafikiri na usawa huu tulionao kumiliki bajaj ni kitu cha mchezo, hili si jambo dogo ni kubwa sana lazima niwashukuru sana na hakika sitoacha kucheza, kwanza ni kampuni iliyo ya kweli na hawana longolongo kwenye kulipa pesa mara unapoweka ubashiri ulio sahihi, mechi zikiisha tu fedha ulizoshinda zinawekwa kwenye akaunti yako papo hapo," aliongeza  Haonga.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya, ushindi ni kwa watumiaji wa mitandao yote ya simu, na mbali ya bajaj, wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali  simu janja (smartphone), jezi halisi za Simba na Yanga pamoja na tiketi ya kushuhudia mechi za Ligi Kuu msimu wa 2018/2019 nchini Uingereza na Hispania.

Sabrina alisema: "Kubashiri na SportPesa ni kwa kila Mtanzania mwenye umri juu ya miaka 18 ambapo kupitia simu yake ya mkononi iwe ya tochi au simu janja anachotakiwa kufanya ni kupiga *150*87# na kisha kuweka pesa namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 baada ya hapo sasa anaweza kuweka ubashiri wake."

Habari Kubwa