Hatima pointi za Azam kitendawili

12May 2016
Faustine Feliciane
Nipashe
Hatima pointi za Azam kitendawili
  • ***Rufaa ya klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es Salaam haijapangiwa siku kwa sababu rufaa iliyokatwa ni ya kawaida na si ya maombi ya dharura...

SHIRIKSHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na klabu ya Azam inayopinga kupokonywa pointi tatu baada ya kubainika ilimchezesha beki Erasto Nyoni akiwa na kadi tatu za njano utatolewa kabla ya Ligi Kuu ya Bara haijafikia ukingoni.

rais tff jamal malinzi

Pazia la Ligi Kuu ya Bara linatarajiwa kufungwa Mei 21 huku tayari Yanga ikiwa imeshatwaa ubingwa.
Azam wamekata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya TFF ikipinga kupokonywa pointi baada ya timu yake kupata ushindi katika mechi hiyo dhidi ya Mbeya City.

Akizungumza jana, Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa kikao cha Kamati hiyo ya Rufaa inayoongozwa na Abbas Tarimba haikijapangwa bado kwa sababu Azam hawakukata rufaa kwa hati ya dharura.

"Kwanza laima ieleweke.., rufaa inakatwa kwa hati ya dharura kama jambo ni la dharura sana, tumepokea rufaa ya Azam kwa hati ya kawaida na tunaifanyia kazi kwa kumpa taarifa Mwenyekiti wa Kamati ambaye yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuitisha kikao," alisema Lucas.

Awali Afisa habari wa Azam FC, Jaffa Iddi alisema wanatarajia maamuzi hayo yatatolewa mapema kulingana na mazingira ya rufaa hiyo.

Habari Kubwa