Juuko aichoka Simba, ataka kusepa

06Mar 2016
Lasteck Alfred
Lete Raha
Juuko aichoka Simba, ataka kusepa

HUKU mkataba wa miaka mitatu wa beki raia wa Uganda, Juuko Murshid na klabu ya Simba ukiwa ndiyo kwanza umeisha miezi 14, beki huyo kisiki amesema kuwa ana mpango wa kwenda kujaribu soka la kulipwa nje ya Afrika ili kujiboreshea maisha yake.

Juuko Murshid

Beki huyo amieleza Lete Raha kwamba ameamua kufanya hivyo kwakuwa kwake mpira ni kazi na kupiga hatua kwenye kazi ni kitu kizuri hivyo hatosita kuondoka pale atakapopata nafasi ya majaribio au dili nje.

“Ninafuraha na kile Simba imenifanyia mpaka sasa, ilinitoa nyumbani Uganda na kunipa nafasi na sasa ninajivunia kwa kile ninachokifanya.

“Hapa si mwisho wangu wa kucheza, nataka kwenda nje kujaribu maisha mengine. Naamini kile ambacho nilitaka kufanya Tanzania nimekitimiza ingawa ubingwa wa Ligi bado lakini ninaishukuru Simba kwa kunilea vyema.

“Kinachonipa moyo ni kuwa Simba ni klabu ambayo imekuwa ikitoa nafasi kwa kila mchezaji kuonesha kile ilichonacho hivyo nitatumia uzoefu na nafasi waliyonipa kupata nafasi nje,” alisema beki huyo wa zamani wa University of Victoria FC.

Juuko ambaye ana miaka 26 kwasasa ameitumikia Simba kwa misimu miwili mfululuzi akiwa moja ya wachezaji wenye nafasi za kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Habari Kubwa