Kabwili akaribia kutimkia Sudan

28May 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR
Nipashe
Kabwili akaribia kutimkia Sudan

KIPA wa Yanga, Ramadhan Kabwili amepata dili na klabu moja ya Sudan na tayari wamefikia mahali pazuri katika mazungumzo na uongozi wa timu ya hivyo, imefahamika.

KIPA wa Yanga, Ramadhan Kabwili

Kabwili alimwambia mwandishi wetu kuwa mkataba wake na Yanga unakamilika Mei 30, mwaka huu na kwamba mbali na ofa hiyo ya Sudan bado anatazama kwingineko.

"Mkataba wangu na Yanga unamalizika mwezi huu, hivyo nina ofa ambazo zipo mkononi tunaendelea kufanya mazungumzo kabla ya kusaini na kuna ni timu moja ya Sudan ambayo tumefika sehemu nzuri," alisema na kuongeza:

"Mazungumzo yakikamilika kila kitu nitaweka wazi ikiwa ni pamoja na timu yenyewe, ila bado sijaikatia tamaa timu yangu ya Yanga kwa kuwa ni sehemu yangu ya kazi na wamenilea pia lazima nitoe kipaumbele kwao."

 

Habari Kubwa