Kamisaa ajitosa kugombea TFF

09Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Kamisaa ajitosa kugombea TFF

KAMISAA wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, Kosuri Osuri, amechukua fomu ya kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuwakilisha mikoa ya Simiyu na Shinyanga.

TFF inatarajia kufanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi mbili za wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo utakaofanyika Februari 2, mwakani huko jijini Arusha.

Nafasi nyingine inayowaniwa katika uchaguzi huo ni ya Kanda ya Mtwara na Lindi, nafasi iliyoachwa wazi na Dustan Mkundi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Osuri, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha mkoa wa Simiyu, alisema ameamua kujitokeza kuwania nafasi hiyo ili kushiriki kikamilifu kusaidia maendeleo ya soka Tanzania.

Habari Kubwa