Kanda arejea kazini Simba

15Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kanda arejea kazini Simba

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Deo Kanda amerejea uwanjani baada ya kuanza mazoezi na timu hiyo kwa ajili ya kujiweka sawa kabla hajarudi rasmi dimbabi kucheza mechi za ushindani.

Akizungumza na Nipashe jana, Kanda alisema tayari amepona na kuanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya kurejea katika ubora wake.
Alisema kabla ya kurejea katika kikosi kuendelea na programu ya timu alifanya mazoezi mepesi ya viungo Gym ambayo anaendelea nayo.

"Namshuku Mungu naendelea vizuri na tayari nimeshaanza mazoezi, na wenzangu baada ya kutoka katika majeraha, suala la kucheza lipo chini ya kocha mwenyewe," alisema.

Kanda aliumia katika mechi ya watani wa jadi, Yanga na kushindwa kuendelea na mchezo huo uliopigwa Januari 4, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Kanda alionekana Kama mashine iliyowaunganisha Simba na alipotoka baada ya kuumia iliwapa nafasi Yanga kupata bao la kusawazisha.

Habari Kubwa