Kaseja agandwa Mbeya City

17Mar 2016
Somoe Ng'itu
Dar
Nipashe
Kaseja agandwa Mbeya City
  • Kipa huyo wa zamani wa Simba na Yanga, yuko kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo ya jiji la Mbeya.

JUMA Kaseja ana nafasi kubwa ya kuendelea kuitumikia Mbeya City FC baada ya uongozi wa klabu hiyo kuvutiwa na kiwango cha kipa huyo.

Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe, aliambia Nipashe kwa simu jana kuwa viongozi wameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kipa huyo katika mechi alizosimama lakoni na kwamba "matokeo mabaya katika baadhi ya mechi ni kawaida ya soka".

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema uamuzi wa mwisho kuhusu wachezaji watakaobaki kwenye cha City kwa ajili ya msimu ujao, yako mikononi mwa kocha mkuu, Mmalawi Kinnah Phiri.

"Kaseja ana nafasi kubwa sana ya kubaki kwenye timu, tulishafanya mazungumzo ya awali, ila sasa hivi tumesimamisha zoezi hilo na umakini umeelekezwa kuisaidia timu ifanye vizuri katika mechi za ligi zilizobaki," alisema.

Meneja wa Kaseja, Athumani Tippo, alisema jana kuea bado wako katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na City.
Agosti mwaka jana, City ilisaini mkataba mfupi wa miezi sita na kipa huyo wa zamani wa Moro United, Simba na Yanga.

Habari Kubwa