KCB yaimwagia Ligi Kuu mil. 500/-

17Sep 2020
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
KCB yaimwagia Ligi Kuu mil. 500/-

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh. milioni 500 za Kitanzania na Bank ya KCB, kwa ajili ya kuongeza nguvu katika msimu wa 2020/21 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Makamu wa Pili wa Rais TFF, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi nchini (TPLB), Steven Mguto, alisema wameingia mkataba kwa awamu ya nne kwa kiasi hicho cha fedha, ambacho wanakiongeza katika mapugufu na sehemu nyingine kukielekeza katika matumizi ya ligi msimu huu.

Alisema huu ni mwaka wa nne wanaingia mkataba na fedha hizo, wataongezea katika sehemu ambayo kutakuwa na mapungufu.

"TFF na Bodi ya Ligi tunafurahi kuona wadau wanajitokeza kusapoti soka la Tanzania, wana imani na sisi na udhamini huo, utaendelea kuleta hamasa na ushindani mkubwa katika ligi yetu," alisema.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa KCM, Barry Chale, alisema wanaendelea kuwa miongoni mwa wadhamini wa ligi baada ya kuthamini sekta ya michezo, ambayo sasa imekuwa ajira kubwa nchini.

Habari Kubwa