Kesi ya Kazimoto yapigwa kalenda

22Mar 2016
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Kesi ya Kazimoto yapigwa kalenda

KESI inayomkabili kiungo wa Simba na Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto imepigwa kalenda na sasa itaanza rasmi kusikilizwa Mei 2 mwaka huu.

Mwinyi Kazimoto.

Kazimoto aliomba kesi hiyo kusogezwa mbele kwa vile ameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars), iliyosafiri kwenda Chad kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika.

Awali, kesi hiyo ya shambulio la mwili dhidi ya mwandishi wa magazeti ya Mwananchi, ilipangwa kusikilizwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga, Rahimu Mushi kabla ya kusogezwa mbele.
Ombi la kutaka kesi hiyo kupangiwa tarehe nyingine lililetwa na wakili wa mchezaji huyo, Paulo Kaunda.

Mwinyi Kazimoto anakabiliwa na tuhuma za kumpiga mwandishi huyo kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Februari 10 mwaka huu.

Mara ya kwanza Kazimoto alipandishwa Kizimbani Februari 22 na kusomewa shtaka hilo na Mwanasheria wa Serikali, Upendo Shemkole. Alikana tuhuma hizo.

Habari Kubwa