Kikapu wasaka Sh. milioni 80

11Mar 2016
Dar
Nipashe
Kikapu wasaka Sh. milioni 80

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linahitaji Sh. milioni 80 kwa ajili ya kuendesha mashindano ya Kanda ya Tano yanayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa kikapu wakifanya mazoezi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji wa Mashindano wa TBF, Manase Zablon alisema fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa ada ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambayo ni dola 20,000 na kiasi kingine kitagharamia mahitaji muhimu ya timu zitakazoshiriki.

"Chama kinahitaji fedha ili kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Kanda ya Tano kama walivyofanya wenzetu Rwanda mwaka jana na ili kupata fedha hizo tayari tumeunda kamati ambayo imeshaanza kufanya mazungumzo na wadhamini," alisema Manase.

Alizitaja nchi zilizothibitisha kushiriki kuwa ni pamoja na Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eritrea, Sudan, Sudan Kusini, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.

Habari Kubwa