Kikwete aiona Tanzania ya michezo

06Nov 2016
Christina Mwakangale
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Kikwete aiona Tanzania ya michezo

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete, amesema uwekezaji kwa vijana katika michezo mbalimbali, Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu katika medani hiyo kwa miaka ijayo.

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete.

Kikwete aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua michuano ya fainali za kwanza za ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana katika Kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park.

Alisema kituo hicho kitatoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 53,000 ili kuwaandaa kucheza mchezo huo ndani na nje ya nchi.

“Wachezaji maarufu duniani kama kina Messi [Lionel], Fabregas [Sesc] walitambuliwa vipaji vyao tangu wakiwa wadogo, ndipo walipofanikiwa kufikia hatua kama hii na kufahamika kimataifa,” alisema Kikwete.

Alisema vijana waanze kutumia fursa iliyopo katika kituo hicho ili vipaji vitambulike na kwamba wadau mabalimbali wamechangia kuwaleta wakufunzi kutoka maeneo tofauti duniani ili kutoa mafunzo.

Naye mmoja wa wachezaji bora wa ligi ya mpira wa Kikapu Marekani kwa upande wa Wanawake (WNBA) Los Angels Sparks, Alana Beard alisema amekuja nchini ili kuwatia moyo vijana ambao wanaibukia katika mchezo huo na kuwaandaa mapema kutasaidia kukuza vipaji vyao.

Katika ligi hiyo, timu zilizoshiriki kutoka shule mbalimbali za jijini ni pamoja na Dar es Salaam International School (DSI), Tusiime na Umoja wa Mataifa.

Habari Kubwa