Kila kona Kigali Niyonzima, Niyonzima

12Mar 2016
Lasteck Alfred
Kigali, Rwanda
Nipashe
Kila kona Kigali Niyonzima, Niyonzima

SI vita, bali ni heshima inayoendelea kutolewa kwa kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kuelekea mchezo wa leo kati ya Yanga na APR.

Niyonzima.

Kinachoshangaza ni kwamba, mashabiki wanaomfuata nahodha huyo wa Rwanda ni mashabiki wa APR.

Kwenye mazoezi ya jana na juzi, mbali na kiungo huyo kupata mapokezi ya kipekee wakati alipowasili na kikosi cha Yanga kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kigali, kiungo huyo mchezeshaji amekuwa gumzo karibu kila sehemu mjini hapa.

Baada ya mazoezi ya jana, basi la Yanga lililazimika kusimama kwa dakika 10 hivi baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuanza kuimba nyimbo zilizokuwa zikitaja jina lake.

“Sina cha kusema, ila nina furaha sana kwa jinsi mashabiki wanavyonikubali na kunipenda.”
Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm alisema: “Ni heshima ya kipekee anayopata Niyonzima. Mashabiki wa hapa wanapenda sana soka.

Habari Kubwa