Kipanga imefanikiwa kutinga fainali hiyo baada ya kuing’oa New King kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu Fainali ya kwanza, huku bao pekee kwenye mchezo huo likifungwa na Mundhiri Abdallah dakika ya 53.
Alisema kuwa kupitia mchezo wa nusu fainali wameona mapungufu kadhaa hivyo wanaenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye fainali.
Alisema kuwa licha ya kutoka na ushindi uliwapelekea kusonga mbele katika michuano hiyo lakini mchezo ulikuwa mgumu katika dakika zote.
“Tumetoka na ushindi na tumetinga fainali ya kwanza kwa Kanda ya Unguja, mchezo ulikuwa mgumu sana na hii ndio maana ya nusu kwa kuwa kila timu ilihitaji kusonga mbele, lakini bahati ilikuwa kwetu na tumesonga mbele,”
“New king japo ni timu ya daraja la kwanza ilicheza vizuri sana na ilisumbua dakika zote 90.”
Kipanga inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili katika Mafunzo na Zimamoto.