Kiwango cha Ngoma chamkuna kocha APR

21Mar 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Kiwango cha Ngoma chamkuna kocha APR

KOCHA wa APR ya Rwanda, Nizar Khanfir amemtaja mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma ndiye alikuwa mwiba na aliwasumbua zaidi katika mechi zote mbili walizokutana na mashindano ya Klabu Bingiwa Afrika.

NGOMA

Akizungumza baada ya mechi yao dhidi ya Yanga juzi, Khanfir, alisema kuwa Ngoma alikuwa na hatari kila alipokuwa na mpira na kumuelezea kuwa ni mchezaji mwenye uzoefu na mashindano ya kimataifa.

"Tulicheza mchezo wa wazi, tulijipanga kushambulia huku pia tukizua lango letu, wachezaji wangu walikuwa na tatizo la kukosa uzoefu na hiyo inatokana na wengi wao bado ni chipukizi, tumeondolewa kwenye michuano hii lakini sasa ni wakati wa kujipanga na mashindano yajayo, bado timu hii tunaijenga," alisema Khanfir aliyejiunga na APR mapema mwezi huu.

Vedaste Kayiranga, makamu wa rais wa Chama cha Soka cha Rwanda (Ferwafa) aliliambia gazeti hili kwamba safari yao ya kusaka ubingwa wa michuano hiyo ilifia Kigali baada ya kukubali kufungwa nyumbani.

Kayiranga alisema APR walicheza kiwango cha chini walipokuwa nyumbani na katika mchezo huo na juzi na walipokuja kuzinduka tayari muda ulishapita.

Habari Kubwa