Tuzo hiyo inayotolewa na Jarida la Ufaransa, France Football na kupigiwa kura na waandishi wa habari waliochaguliwa duniani kote, haikufanyika mwaka jana kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona.
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Lewandowski alimaliza nafasi ya pili huku Salah wa Liverpool akimaliza nafasi ya saba.
Kocha wa Liverpool, Klopp ameibuka na kusema kuwa Messi amependelewa dhidi ya Lewandowski na Salah.
"Sina uhakika kwa asilimia 100 kuhusu tuzo ya Ballon d'Or," alisema Klopp wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
"Mara zote anapewa Messi na sina tatizo na hilo, lakini kama huwezi kumpa Robert Lewandowski wakati huu baada ya kuwa na mwaka bora, kwa hakika kabisa inashangaza.
"Na Mo (Salah) alitakiwa kuwa kwenye nafasi ya juu zaidi. Ilishangaza na nafasi aliyokuwapo.
“Niliona kura sehemu moja, sijui namna gani wanapiga hizo kura. Ni waandishi wa habari, sidhani, sina uhakika sana kwa hilo.”