KMKM, Mafunzo, Zimamoto zapeta

06Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Zanzibar
Nipashe Jumapili
KMKM, Mafunzo, Zimamoto zapeta

JUMLA ya mabao 452 yamefungwa katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliomalizika Desemba 31 mwaka jana.

Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Ali Mohammed akimpita beki wa Timu ya KMKM Said Hamza wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar

Mabao hayo yamefungwa katika mechi 171 zilizochezwa katika viwanja mbalimbali vilivyoko Unguja na Pemba, huku kila timu ikicheza mechi zake 18.

Timu tatu ambazo zinaongoza kwa kufunga mabao katika mzunguko huo wa kwanza ni pamoja na KMKM wenye magoli 40, Mafunzo wao wamepachika wavuni mabao 35 huku Zimamoto yenye mabao 34 ikishika nafasi ya tatu.

Taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) jana inasema kuwa timu sita kati ya klabu 19 zinazoshiriki ligi hiyo zitashuka daraja wakati timu  itakayopanda itakuwa moja na kuufanya msimu ujao kushirikisha timu 14 tu.

Timu zinazoshiriki ligi hizo ni pamoja na vinara KVZ, JKU, KMKM, Mafunzo, Malindi, Mlandege, Chuoni, Polisi, Jang’ombe Boys, Zimamoto,  Mwenge, New Star, Jamhuri, Selem View, Mbuyuni, Hard Rock, Opec, Kizimbani na Chipukizi.

Habari Kubwa