Kocha Yanga aishusha presha

26Jun 2018
Faustine Feliciane
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kocha Yanga aishusha presha

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na kwamba anakiandaa kikosi kitakachorejesha furaha yao.

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Zahera, ambaye alikuwa kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa sasa ameanza kukisuka kikosi chake huku akiwa na majina ya nyota anaowataka kuwaongeza kwenye kikosi hicho.

Mcongo huyo aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa wachezaji atakaowasajili ana uhakika watarudisha makali ya timu hiyo.

“Hakuna shaka, naandaa timu ambayo itakuwa na ubora, lengo ni kuhakikisha timu inakuwa ya ushindani,” alisema Zahera.

Alisema hata usajili atakaoufanya utazingatia mahitaji ya timu yake.

“Tunasajili kulingana na mapungufu ambayo nimeyaona kwenye timu, lazima tufanye kazi kama timu, kwa kushirikiana na viongozi na wachezaji wenyewe naamini timu itakuwa bora zaidi msimu ujao,” alisema Zahera.

Alisema kwa sasa licha ya kuwa katika mchakato wa usajili, lakini pia wanaupigia mahesabu mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya utakaopigwa nchini humo Julai 18, mwaka huu.

Habari Kubwa