Kombe la Europa League laibiwa huko Mexico

22Apr 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kombe la Europa League laibiwa huko Mexico

Kombe la Europa League ambalo linashikiliwa na klabu ya Manchester United iliyolitwaa msimu uliopita, limeripotiwa kuibwa kwenye gari lililokuwa likitumiwa kulisafirisha huko Mexico lakini limepatikana baada ya msako mkali.

Kombe hilo liliibiwa usiku wa ijumaa kuamkia Jumamosi muda mfupi baada ya kuoneshwa kwenye uwanja wa soka huko mjini Leon jimbo la Guanajuato lakini maafisa wa usalama walifanikiwa kulipata jana hiyo hiyo.

Afisa usalama wa jimbo la Guanajuato ameujulisha Umma kuwa Kombe hilo limepatikana na liliibiwa kwenye gari ambayo inatumika kusafirisha Kombe hilo kwenye maonesho katika miji mbalimbali.

Kampuni ya magari ya FedEx ndio inatumika kusafirisha kombe hilo na ndio wadhamini wakuu wa michuano ya Europa msimu huu hivyo wanatumia maonesho hayo kuongeza wafuasi wa michuano hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa kombe la soka duniani kuibiwa ambapo imewahi kutokea mwaka 1966 Kombe la dunia liliibiwa jijini London, Uingereza, lakini likapatikana baadaye.

 

Habari Kubwa