Kombe la Shirikisho rasmi Novemba 19

06Nov 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Kombe la Shirikisho rasmi Novemba 19

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetangaza michuano ya Kombe la Shirikisho itazinduliwa rasmi Novemba 19, mwaka huu mkoani Tanga.

Afisa-Habari-wa-TFF-Alfred-Lucas.

Michuano hiyo kwa mwaka huu itashirikisha timu 86 ikiwa ni timu 22 zaidi ya zile zilizoshiriki mwaka jana, na siku ya ufunguzi watashuhudiwa mabingwa wa Mkoa wa Tanga, Muheza United wakiumana na Sifa Politan ya Temeke, Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mkwakwani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TFF, kabla ya mchezo huo wa ufunguzi, kutakuwa na shamrashamra mbalimbali zitakazokuwa zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo, Kampuni ya Azam Media.

Katika timu hizo 86 zitakazoshiriki, 16 ni za Ligi kuu, 24 za Ligi Daraja la Kwanza, 24 za Ligi Daraja la Pili pamoja na 22 za mabingwa wa mikoa huku michuano hiyo ikipangwa kuendeshwa kwa mizunguko tisa kabla ya kumpata bingwa ambaye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2018.

Wakati huo huo, Ligi ya vijana wenye umri wa miaka 20 ya TFF imepamgwa kuanza Novemba 15 na uzinduzi wake utafanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kwa kushuhudia Kagera Sugar wakicheza na Yanga.

Habari Kubwa