Kufuzu Olimpiki kufanyika Misri

16Jan 2019
Renatha Msungu
Dar es Salaam
Nipashe
Kufuzu Olimpiki kufanyika Misri

MASHINDANO ya mchujo ya soka kwa ajili ya kufuzu kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki imepangwa kufanyika mwakani nchini Misri.

Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika nchini Zambia lakini kwa sasa yamepangwa kufanyika Misri huku sababu ya kuhamisha nchi zikiwa bado hazijatajwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau, alisema mashindano hayo yamepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

"Mashindano ya kufuzu rasmi kwa michezo hiyo inaanza mwakani kwa upande wa soka na michezo mingine,"alisema Tandau.

Aidha, akizungumzia kuhusiana na uwenyeji wa mkutano wa makatibu wote kamati za Olimpiki, alisema mkutano huo umepangwa kufanyika Aprili mwakani visiwani Zanzibar.

Alisema wao kama wenyeji wanafurahi kupata fursa hiyo kwa sababu ni moja ya nafasi ya wao kuitangaza nchi na vivutio vyake.
Alisema wanatarajia kuanza mapema maandalizi ya kuandaa mkutano huo mkubwa na wanaamini watafanikiwa.