Kuogelea taifa kuchuana Aprili

16Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kuogelea taifa kuchuana Aprili

MASHINDANO ya kutafuta bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea yamepangwa kufanyika Aprili 7 na 8, mwaka huu kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Heaven of Peace Academy (Hopac) iliyopo Kunduchi Mtongani.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alizitaja timu ambazo zinatarajia kushiriki kuwa ni Dar es Salaam Swimming Club, Taliss swimming Club, Bluefins, JKT, Morogoro International School, Champions Rise, Braeburn International School na shule ya sekondari ya Makongo.

Timu nyingine ni ISM Leopards, Arusha Swim Club, Mwanza Swim Club, Kennedy School Arusha, Stingrays Swim Club, Tanzania Marines, Hopac Swim Club, Genesis Swim Club, KMKM, Wahoo –IZS na Zanzibar Dolphins.

“Tunatarajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ya kila timu, mchezo unakua na timu zinazidi kuongezeka, kwa kifupi kuna mwamko mkubwa sana katika mchezo, tunawaomba wadhamini wajitokeze kutusaidia,” alisema Namkoveka.

Habari Kubwa