Kuogoela kusaka medali kesho

09Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kuogoela kusaka medali kesho

TIMU ya taifa ya kuogelea kesho wanataanza harakati za kusaka medali kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.

magdalena moshi.

Mchezaji wa timu hiyo, Magdalena Moshi, aliliambia Nipashe kwa njia ya mtandao kuwa wamejiandaa vyema kutupa karata yao kwa kwanza kwenye michezo hiyo.

"Tunaomba watanzania watuombee kwa na sisi tutapambana kuhakikisha safari hii tunafanya vizuri," alisema Magdalena.

Alisema kocha wao, Alex Mwaipasa amewapa mbinu ambazo zitawafanya kushindana kwenye michezo hiyo.

Timu hiyo ya kuogelea itashiriki kwenye mchezo wa kwanza kesho kwa mtindo huru 'Free Style'.

Mchezaji wa judo Andrew Thomas jana usiku alitarajiwa kupanda ulingoni kwenye michezo hiyo akipigana kwa uzito wa kilo 75.