Lady Jay Dee kutikisa Dodoma Idd El-Haji

30Aug 2017
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Lady Jay Dee kutikisa Dodoma Idd El-Haji

MSANII wa Muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee, anatarajiwa kutoa burudani ya nguvu mkoani hapa, Septemba Mosi, mwaka huu katika tamasha la uzinduzi wa eneo la Kisasa la burudani, Capetown Complex.

Lady Jay Dee.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, msanii huyo alisema wapenzi wa muziki watarajie shoo nzuri kutoka kwake na kwa wasanii wenzake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Capetown Entertaiment, Frank Ngonyani, alisema wameamua kuandaa tamasha kubwa, ili kuwapa burudani wakazi wa Dodoma na viunga vyake.

Ngonyani alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.

Alibainisha kuwa, kabla ya uzinduzi huo, utatanguliwa na mbio la kilomita tano za watu wenye ulemavu wa ngozi ambao watapatiwa mafuta, kofia na miwani, ili kujikinga na mionzi ya jua.