Lewandowski ni suala la muda tu Barcelona

29Jun 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Lewandowski ni suala la muda tu Barcelona

RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, Javier Tebas amekiri angependa kuidhinisha uhamisho wa Barcelona kumnunua Robert Lewandowski, lakini shughuli hiyo inategemea kama Blaugrana hao watakidhi 'vigezo' vya kiuchumi katika siku chache zijazo.

Rais wa Barcelona, Joan Laporta aliongoza mkutano wa wanachama wa Klabu hiyo wiki iliyopita ambapo alifichua mpango wa kurudisha nguvu za kiuchumi ambazo zitasaidia kupunguza upotevu wa kifedha ulitokea msimu wa 2021/22 na kuwawezesha kufanya usajili wa fedha nyingi msimu huu wa joto.

Mlengwa namba moja wa Barca bado ni Lewandowski, ambaye mwezi uliopita alisema hadharani kuwasihi Bayern Munich kumruhusu kuhamia Katalunya kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka ujao.

Tebas, mkosoaji anayejulikana wa shughuli za kifedha za Barcelona katika miaka michache iliyopita, amekiri kuwa angeidhinisha dili la Lewandowski ikiwa ni muhimu kwa klabu hiyo.

"Ninatumaini kwamba Lewandowski atachezea Barcelona na ana msimu mzuri. Ninatumaini kwamba, wale wawezeshaji wa kifedha ambao Laporta anawatumia watamfikisha Barcelona, ​​kwa sababu ni gwiji wa Bayern Munich na soka la Ulaya," alisema Tebas.

"Ikiwa kile walichokiidhinisha wanachama kitatekelezwa, ataweza kuichezea Barcelona. Kuna maslahi na kama watatekeleza hatua hizo wataweza kumsajili."

Habari Kubwa